BARAZA LA MITIHANI LA TANZANIA
RATIBA YA MTIHANI WA KIDATO CHA SITA MWAKA 2015 HAIJABADILIKA Baadhi ya watu wamekuwa wakitumiana ujumbe kwenye mitandao ya kijamii wenye kupotosha kwamba Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi ametangaza kuwa Mtihani wa Kidato cha Sita (ACSEE) 2015 utafanyika kuanzia tarehe 2 hadi 25 Machi 2015 badala ya tarehe 4 hadi 27 Mei 2015. Aidha, ujumbe huo umetoa sababu kuu ya mabadiliko ya ratiba ya mtihani kuwa inatokana na mwingiliano wa ratiba ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015 na mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT). Baraza la Mitihani la Tanzania linapenda kuwafahamisha watahiniwa wa Mtihani wa Kidato cha Sita 2015 na umma kwa ujumla kuwa taarifa hizo ni za UONGO na zinalenga kuupotosha umma wa watanzania. Baraza linapenda kusisitiza kuwa ratiba ya Mtihani wa Kidato cha Sita 2015 HAIJABADILIKA na kwamba Mtihani huo utafanyika kuanzia tarehe 4 hadi 27 Mei 2015 kama ilivyopangwa awali, Baraza la Mitihani linaomba wadau wazipuuze taarifa hizi zinazosambazwa kwenye mitandao ya kijamii kwa kuwa zina lengo la kupotosha umma. Imetolewa na,
AFISA HABARI NA UHUSIANO
for more infomation click here www.necta.go.tz
ZANZIBAR COMMERCIAL SECONDARY SCHOOL
Wednesday, January 14, 2015
TANGAZO
BARAZA LA MITIHANI LA TANZANIA
Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani la Tanzania anapenda kuwatangazia watu wote wanaotaka kufanya Mtihani wa Kidato Cha Nne (CSEE) na Maarifa (QT) Mwezi Novemba 2015 kwamba usajili umeanza rasmi tarehe 01 Januari 2015. Watahiniwa watakaojisajili katika kipindi cha kawaida yaani tarehe 01 Januari 2015 hadi 28 Februari 2015 watalipa ada ya Shilingi 50,000/- kwa wanaojisajili mtihani wa Kidato cha Nne (CSEE) na Shilingi 30,000/- kwa wanaojisajili mtihani wa Maarifa (QT). Watahiniwa watakaojisajili kwa kuchelewa yaani kuanzia tarehe 01 Machi 2015 hadi tarehe 31 Machi 2015 watalipa ada ya Shilingi 65,000/ kwa Kidato cha Nne na ada ya Shilingi 40,000/- kwa mtihani wa Maarifa (ada pamoja na faini). Waombaji wote watajisajili kwa njia ya mtandao kupitia tovuti ya Baraza la Mitihani: www.necta.go.tz. Kabla ya kujisajili kwenye mtandao waombaji watapaswa kwenda kwenye vituo wanavyokusudia kufanyia mtihani kuchukua namba rejea (Reference Number). Wakuu wote wa vituo nchini wamekabidhiwa namba rejea na watazigawa kwa watahiniwa tarajali bila malipo. Aidha waombaji watapaswa pia kulipa ada ya mtihani kwa njia ya Posta au M-Pesa kabla ya kujisajili kwani hakuna mtahiniwa atakayeweza kujisajili bila kulipa ada ya mtihani. Waombaji wote wazingatie kwamba kipindi cha usajili kitafungwa rasmi tarehe 31 Machi 2015 Imetolewa Na: KATIBU MTENDAJI

for more information click here www.necta.go.tz
Subscribe to:
Posts (Atom)